Wakenya waadhimisha miaka 25 ya wimbo wa 'Stella Wangu' wa Freshley Mwamburi
Wakenya
walilazimika kuuchangamkia wimbo huo wakikumbuka tukio lililowahi kutokea tarehe
17/5/1992 wakati mpenzi mwanamke mmoja ajulikanae kama, Stella, aliposhuka
kutoka kwa ndege na mchumba wake wa urefu wa futi nne Mjapani, huku amebeba
mtoto mkononi.
Kisa
hicho cha kweli kilichomtokea Freshley, jana kilikuwa kikifikisha miaka 25
tangu siku hiyo. Freshley anasema alitaka tu kuthibitisha ni kweli Stella
ameamua kuolewa na mwalimu wake huyo huko Japan alikoenda kusomea utabibu.
Wakenya
wametuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, wengine wakimkashifu Stella kwa
kumtumia vibaya Freshley, ambaye alilazimika kuuza mifugo na shamba lake ili
Stella apate nauli ya kwenda Japan kusoma.
Lakini sasa
Freshley amesahau yote hayo, na bado anawasiliana kwa simu na Stella akiwa
Tokyo, Japan, lakini anasema hamna lolote la kimapenzi ila ni kujuliana hali
tu. Stella sasa ana watoto wawili, naye Freshley ameoa na ana watoto wanne -
wavulana watatu na msichana mmoja.
Katika wimbo wake, Freshley aliimba:
"Nilikua na mchumba wangu, tulipendana kama
nyama choma
Alibahatika kwenda ngambo, chuo kikuu kwenda
kusoma, miaka mitatu kule Japani kusomea udakitari, Stella wangu ehhh.
Nilivyompenda Stella jamani kajitolea kwa roho
moja, nikauza shamba langu, sababu yake yeye,
Nikauza gari langu, sababu yake yeye nikauza
Ng'ombe na mbuzi sababu yake yeye,
Ili apate nauli ya ndege na pesa nyngine za
matumizi kule Japani,
Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano, ilikua
tarehe kumi na saba mwezi wa tano, ndiyo ilokua tarehe kamili ya Stella kurudi
Kenya.
Nilikwenda uwanja wa ndege kwenda kumlaki Stella,
nilikua na uncle (mjomba/au rafiki) Kilinda uwanja wa ndege,"
"Ghafla ndege ilipotua uwanajani tuliona
vituko, Stella alishuka amebeba mtoto mkononi, nyuma yake mchumba wake mfupi,
futii nne Mjapani,
Nilisikitika ndani ya moyo nikakosa la kufanya,
Nilitamani nilie Kikamba lakini si kijui, ilibidii
nilie Kijaluo "angatima ngo wachoa",
Freshley, nilitamani nilie Kihindi lakini si kijui,
ilini bidii nilie Kitaita lugha ya mama na baba,
ilinibidi nilie Kitaiaa, "beke mwana niponyebanda,
Freshley".
Usikilize
mwenyewe
No comments