Header Ads

Nipo tayari kujitoa mazungumzo ya Brexit - May



Theresa May aliingia madarakani mwaka 2016 baada ya aliyekuwa waziri mkuu David Cameron kujiuzulu kwa kushindwa kuzuia kujitoa kwenye umoja wa Ulaya
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu, Theresa May amesema kuwa yupo tayari kutoka nje na kuachana na mazungumzo kuhusiana na kujitoa katika Jumuiya ya Ulaya (EU), iwapo tu kutakuwa na makubaliano mabaya.

Alisema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano maalum, ambayo yalirushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya Sky News, na Channel Four.
May alisisitiza kuwa watakuwa pale kujadiliana makubaliano mazuri, na kusema kuwa ni bora kutokuwa na makubaliano, kuliko kuwa na makubaliano mabaya.
Katika mahojiano hayo, Jeremy Corbyn alikabiliwa na maswali magumu kuhusiana na uhusiano wake wa zamani na makundi ya wapiganaji ya Ireland na mashariki ya kati. Alikosolewa pia kutokana na kuhudhuria tukio la wanachama wa IRA mwaka 1987
Uingereza inatakiwa kujitoa kutoka EU ndani ya miaka miwili kwa mujibu wa utaratibu.

No comments

Powered by Blogger.