Marekani kujaribu kutungua makombora ya masafa marefu

Makombora ya Korea Kaskazini ambayo yamekuwa yakijaribiwa kila mara na kuleta hofu Marekani.
WASHINGTON DC, Marekani
IDARA ya Jeshi nchini, kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la
masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi bara
lingine.
Maofisa wa Pentagon wanasema jaribio hilo litafanyika Jumatano, wiki
ijayo. Hayo yanajiri, baada ya kuwepo kwa wasiwasi kuhusu uboreshaji wa miradi
ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini.
Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani, alisema iwapo miradi ya Korea
Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo
wa kutengeneza kombora lenye uwezo wa kufika Marekani.
Matamshi hayo yanaonesha wasiwasi wa Marekani kuhusu mpango wa Korea
Kaskazini, wa kutengeza makombora ya mbali na mpango wake wa kinyuklia, ambayo taifa
hilo inasema inahitaji kwa ulinzi wake.
Maofisa wa Serikali, walisema kuwa majaribio hayo yalipangwa mapema na
kwamba haijibu kisa chochote. Pentagon ilitangaza jaribio hilo wakati ambapo
Korea Kaskazini inatengeza kombora la masafa marefu.
Ni mara ya kwanza kwa Marekani kujaribu kuzuia kudungua kombora la
masafa marefu ICBM. Marekani imekuwa ikitumia kifaa cha GMD kinachowekwa
ardhini, kukabiliana na mashambulio ya mataifa kama vile Korea Kaskazini.
Kifaa hicho kina uwezo wa kudungua makombora mengine, lakini
hawajajaribu kudungua makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kurushwa
kutoka bara moja hadi jingine.
Huku maofisa wa Marekani wakiamini kwamba Korea Kaskazini ina miaka
mingi ya kuweza kufanikiwa kutengeza kombora la masafa marefu la ICBM, lakini wanaamini
taifa hilo limepiga hatua.
No comments