Griezman: Ninaweza nikahamia Man United
Nyota wa klabu ya
Atletico Madrid Antoine Griezman ambae amekua akihusishwa na kuhamia katika
timu ya Manchester United amesema inawezekana uhamisho huo ukafanyika katika
dirisha kubwa la usajili
Griezman (pichani) akihojiwa katika kipindi cha Television huko nchini Ufaransa
amesema uhamisho huo unawezeka kwa asilimia 6 kati ya 10.
“Nafikiri nitaamua
kuhusu hatma yangu wiki mbili zijazo,” alisema nyota huyo wa timu ya klabu ya
Atletico Madrid, iliyo chini ya Diego Simeone.
Mchezaji huyu ameichezea timu ya taifa ya Ufaransa michezo 41 tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwak 2017 na amefunga jumla ya mabao 26 mismu huu akiwa na timu yake ya Atletico iliyomaliza ligi katika nafasi ya tatu.
No comments