Dogo Mfaume wa ‘kazi yangu ya dukani’ afariki dunia
TASNIA ya Bongo Fleva imepatwa na
msiba, baada ya msanii aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Kazi yangu ya Dukani’
anayejulikana kwa jina la Dogo Mfaume kufariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chanzo
cha kuaminika, Dogo Mfaume amefia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
alikokuwa akitibiwa.
Taarifa hizo zinaeleza kwamba, Dogo Mfaume
alikuwa akisubiri kufanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa ili kuondoa uvimbe uliokuwa
kwenye ubongo kichwani mwake.
Mmiliki wa Sobber House alikokua
akisaidiwa ili kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya amesema ‘alikua afanyiwe
upasuaji Ijumaa kutokana na uvimbe kwenye ubongo na alikua tayari ameshapangwa
kwenye ratiba’
‘Afya yake ilikua nzuri kabisa na
alikua ana mwaka mmoja toka ameacha utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ na
tulikua tumejiandaa kesho twende tukamtolee damu’
Akiongea huku analia Mmiliki huyo wa Sobber House alisema
kwamba; “Afya yake ilikua nzuri kabisa na aliniambia dada mimi sitaki kuondoka
kwako, nataka unisimamie kila kitu na sitaki kurudi mtaani, mtaani hali mbaya
na nikikaa kule nitarudi kutumia unga”
No comments