Header Ads

Trump atoa masharti mapya ya Visa



Rais Donald Trump wa Marekani ametoa masharti mapya
WASHINGTON DC- UTAWALA wa Rais Donald Trump, umeweka masharti mapya ya maombi ya Visa kutoka kwa mataifa sita ya Kiislamu pamoja na wakimbizi wote, ambayo yanawataka kuwa na ndugu au mshirika wa kibiashara nchini.

Hatua hiyo inayahusisha mataifa yalio na Waislamu wengi kama vile Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen na tayari ujumbe umeshatumwa kwenye balozi zote za mataifa hayo na balozi za Marekani katika mataifa hayo.
Masharti hayo mapya yanayoanza kufanya kazi leo, yanaelezea mahusiano ya kifamilia kama mzazi, mkeo ama mumeo, mtoto wa kiume ama wa kike ndiye anapaswa kuwapo nchini.
Masharti hayo yanajiri baada ya Mahakama Kuu nchini, kuidhinisha kwa muda agizo la Rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa Waislamu.

No comments

Powered by Blogger.