‘Marufuku kutuma sms kwa lugha za asili Kenya’

NAIROBI- VYAMA vya Siasa nchini, vimeagizwa
kusitisha mara moja au kufuta mipango yao ya kutuma jumbe fupi zilizoandikwa
kwa lugha za asili kwa njia za simu kwenda kwa wananchi.
Jumbe hizo ambazo zimekuwa zikitumwa moja kwa moja
kwa watu wengi, zimeelezwa kuwa ni zinachochea chuki na kusababisha kukithiri
kwa ukabila na kurudisha nyuma juhudi za Serikali kukomesha ukabila.
Sheria hizo mpya ambazo zimezotelewa na Serikali
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA), pamoja na Tume ya Ushirikiano ya
Taifa (NCIC) zinaeleza kwamba jumbe hizo zinapaswa kutumwa kwa lugha mbili tu
ambazo ni Kiswahili na Kingereza.
Hayo yanajiri katika kipindi ambacho wanasiasa
wameshikwa vikali na homa ya uchaguzi, ambao unatarajiwa kufanyika Agosti 8,
mwaka huu ili kuwazuia wanasiasa hao kutumia majukwaa yao kwenye mitandao ya
kijamii na simu kueneza chuki.
Chini ya sheria hizo kali, wakala wa kusimamia maudhui
wamewaandikia barua rasmi za kuzitaka kampuni simu kubainisha chama au vyama
vinavyosambaza jumbe za chuki na zilizoandikwa kwa lugha za asili.
No comments