Header Ads

Kadinali matatani kwa unyanyasaji wa kingono



Kadinali George Pell akiwa Vatican
MELBOURNE- POLISI nchini, imemshitaki Kadinali wa Kanisa Katoliki mwenye ushawishi mkubwa, George Pell, kwa makosa kadhaa ya kuwanyanyasa watoto kingono.

Kadinali Pell (pichani) amekanusha makosa hayo ambayo yanasemekana kufanyika miaka ya 1970. Anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama mjini hapa Julai mwaka huu.
Licha ya mashtaka hayo dhidi ya mtumishi wao, wawakilishi wa kanisa hilo hawajatoa tamko lolote juu ya suala hilo licha ya BBC kutoa ombi la kuwataka kufanya hivyo.
Idara ya Polisi, iliamua kuchukua hatua ya kumfungulia mashtaka Kadinali Pell, baada ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi wa mashtaka mwezi uliopita.
Naibu Kamishna wa polisi, amesema mchakato wa kumfungulia mashtaka kadinali huyo hauna tofauti yoyote na uchunguzi wowote.
Kadinali Pell ni Mwekahazina wa Vatican na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini.  Maofisa wa polisi wa jimbo la Victoria, wamesema mashtaka hayo yanatokana na madai ya ‘kihistoria’.
“Madai hayo yalitolewa na zaidi ya mtu mmoja” alisema naibu kamishna wa polisi, Shane Patton. Kadinali Pell ambaye makao yake makuu yako Vatican, amekana madai hayo.
Akiwa mwekahazina wa Vatican, Kadinali Pell anatambulika kuwa ofisa wa tatu mkuu katika kanisa hilo.
Katika taarifa iliyotolewa na kanisa hilo, Kadinali Pell atarudi nchini haraka iwezekanavyo, ili kujisafishia jina lake kufuatia ushauri ulioungwa mkono na madktari wake ambao pia watamshauri kuhusu mipango yake ya kusafiri.
Alisema kuwa yuko tayari kufika mahakamani na atajitetea mashtaka yanayomkabili.
Kadinali huyo siyo mkuu wa kanisa hilo nchini, bali pia ni miongoni mwa viongozi wakuu walio na hadhi ya juu katika ulimwengu wa kanisa hilo.
Katika kipindi cha miongo miwili, amekuwa amekuwa katika mstari wa mbele katika mjadala wa kanisa hilo kuhusu masuala tata kama vile lile la wapenzi wa jinsia moija, ukimwi na utafiti wa seli.
Pia amehusika katika kutoa majibu ya kanisa hilo kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kingono nchini.

No comments

Powered by Blogger.