Italia yatishia kuzuia wahamiaji kuingia pwani zake
Mwakilishi
wa taifa hilo katika jumuiya ya mataifa ya bara Ulaya, Maurizio Massari,
ameonya kuwa idadi ya wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterranea kutoka Afrika Kaskazini
inazidi kuongezeka.
Karibu
watu 10,000 wameripotiwa kujaribu safari hiyo siku chache zilizopita.
Awali
kamishna wa masuala ya uhamiaji ya EU, Dimitris Avramopoulos, alisema mataifa
yote wanachama wa EU yalikuwa na jukumu la kibinadamu la kuokoa maisha na
kwamba hayangeweza kuachia jukumi hilo mataifa machache kakabiliana na suala
hilo.
Mataifa
28 wanachama wa jumuiya hiyo wametoa chini ya nusu ya Euro milioni 200 waliyoahidi
kukabiliana na wahamiaji kutoka Afrika, hususan Libya ambako ndiko kituo kikuu
cha mwanzo wa safari.
No comments