Amir wa Dubai asaidia kuwanunulia kanisa wanakijiji
Wakazi
wa eneo la Godolphin karibu na Helston, walimtumia ujumbe kwa lengo la kufanya
mchango. Kijiji hicho kina jina linalofanana na Godolphin Stables
kilichoanzishwa na Sheikh huyo kulingana na Cornwal.
Richard
Mackie kutoka muungano wa jamii ya Godolphin Cross alisema: “Tunamshukuru sana”.
Kundi
hilo lilihitaji pauni 90,000 (sh milioni 198) kulinunua kanisa hilo, ambalo
walitaka kulibadilisha na kulifanya kituo cha jamii na walikuwa wamechangisha
pauni 25,000.
Haijulikani
ni kiwango gani cha fedha kilichotolewa na Sheikh Mohammed, lakini Mackie
alisema ‘ametusaidia sana’.
Mwanakijiji
mmoja, Valerie Wallace alikuwa na wazo hilo kama hatua ya mwisho baada ya kundi
hilo kushindwa kuchangisha fedha kutoka maeneo mengine.
“Hatukufikiria
wazo kama hilo, lakini baadaye tukaanza kupata simu kutoka Abu Dhabi. Tulidhani
tulikuwa tunafanyiwa mzaha lakini baadaye tukagundua sio kamwe,” alisema Mackie.
No comments